Mwanza, Tanzania
La madre empezó a tener dolores de parto a la 1 de la madrugada. Su marido estaba de viaje así que fue a buscar ayuda a los vecinos y los acompañó a caminar hasta la parada de taxis pero no pudo hacerlo porque el dolor era demasiado y se detuvieron en el campo de fútbol. El hombre fue a buscar ayuda, pero cuando volvió ella ya había dado a luz: el cordón estaba siendo cortado pero la placenta no había salido y ella sangraba mucho. «Tal vez ese era mi día para morir», dijo que pensaba. Uno de los conductores de boda boda pasó por allí y se detuvo, envió un mensaje de texto pidiendo ayuda y los bomberos acudieron al transporte.
Mnamo saa saba usiku,Mama mjamzito alianza kuhisi uchungu wa kujifungua. Mume wake alikuwa amesafiri hivyo ikabidi aende kwa majirani ili kutafuta msaada wa kwenda kutafuta taxi ya kumpeleka hospitali lakini hakuweza kutokana na kuzidiwa uchungu na kushindwa kutembea ilibidi wamkalishe kwenye kiti kilichokuwa katika uwanja wa mpira. Jirani aliekua akimsaidia alienda kutafuta msaada na hatimae aliporudi akakuta yule mama tayari kajifungua pale kwenye kiti, kitovu kilikuwa kishakatwa lakini kondo la nyuma lilikuwa bado halijatoka na damu ilikua inatoka sana.»Labda siku ile ilikuwa siku yangu ya kufa» yule mama alisema. Mmoja kati ya waendesha boda ambaye ni mtoa huduma ya kwanza aliekua akipita, alisimama na kupiga simu kituo cha zima moto na hatimae gari lilifika na kuwapeleka hospitali yeye pamoja na mwanae.